Jumapili, 8 Februari 2015

SPURS YASHINDA DERBY YA LONDON





Harry Kane aliendelea kuimarika baada ya kuifunga Arsenal mabao mawili huku Tottenham ikitoka nyuma na kuibuka kidedea kwa mabao 2-1 katika mechi ya London Derby. Kane alifunga baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Mousa Dembele aliyegusa krosi ya kona mapema katika kipindi cha pili. Baadaye alifunga kichwa kizuri katika dakika ya 86 na kuiweka Spurs juu ya Gunners katika jedwali la ligi ya Uingereza

 . Mesut Ozil aliiweka Arsenal kifua mbele katika kipindi cha kwanza laki mshambulizi yasio koma ya Tottenham katika ngome ya Arsenal yalizaa matunda na kuiweka Tottenham kuibuka kidedea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni