Jumapili, 8 Februari 2015

ANGALIA BEKI HUYU ALIVYOKABA HADI SURA


 Mchezaji Robbie Neilson alijikuta kwenye maumivu makubwa baada ya kulambwa kiatu cha uso kutoka kwa nahodha wa timu ya Livingston, Jason Talbot.
Hiyo ilitokea wakati Livingston ikipambana na Hearts katika Ligi ya Scotland.
 Nicholson alilazimika kupata matibabu na kushonwa nyuzi kadhaa baada ya buti hilo la Talbot.
Walikuwa wanawania mpira wa juu, wakati Neilson akiruka kupiga kichwa, Tailbot alipeleka mguu na kumjeruhi vibaya.

KOCHA WA SIMBA ATUMA MAOMBI KWA MASHABIKI WA SIMBA


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kuna kila sababu ya mashabiki wa Simba kuendelea kumvumilia.


Amesema ana imani na kikosi chake kitakuwa na mabadiliko baada ya muda, lakini uvumilivu ndiyo dawa.
“Tumekuwa na vipindi vya kupanda na kushuka, utaona mechi moja tuko bora zaidi na nyingine tunashuka.

“Uvumilivu ndiyo jambo muhimu zaidi. Hatuwezi kufanikiwa kama leo tutachanganyikiwa na kuanza kufanya vitu nje ya msitari.
“Sare na Coastal si tulichokitaka, lakini angalau hatujapoteza mchezo tunaweza kuendelea kujipanga,” alisema Kopunovic raia wa Simba.

PLUIJM AWAPA DAWA WACHEZAJI WA YANGA KABLA YA KUIVAA YANGA LEO TAIFA



Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia wachezaji wake, dawa ya kuondokana na kupoteza nafasi nyingi ni kuwa watulivu na kuachana na presha ya mashabiki kwa muda.


Pluijm raia wa Uholanzi, ameendelea kulizwa na wachezaji wake kupoteza nafasi za kufunga na kusema wanaweza kuzitumia vema kama wakijiondoa katika presha.

"Wachezaji wanachanganyikiwa kwa kuwa presha ni kubwa sana, wako wanataka kufunga kila mpira lakini wako ambao wanapata nafasi, lakini hawana utulivu.

"Yanga ni timu kubwa, presha ya mashabiki ipo juu na hii inawaathiri wachezaji.

"Nimezungumza nao mara kadhaa, nimesisitiza suala la presha na kuwaambia mashabiki wana haki yao katika kudai ushindi na mabao lakini wao wanapaswa kufanya kazi yao kwa ufasaha kwa mujibu wa tulichojifunza," alisema.

Yanga inashuka leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kucheza mechi yake ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.


SPURS YASHINDA DERBY YA LONDON





Harry Kane aliendelea kuimarika baada ya kuifunga Arsenal mabao mawili huku Tottenham ikitoka nyuma na kuibuka kidedea kwa mabao 2-1 katika mechi ya London Derby. Kane alifunga baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Mousa Dembele aliyegusa krosi ya kona mapema katika kipindi cha pili. Baadaye alifunga kichwa kizuri katika dakika ya 86 na kuiweka Spurs juu ya Gunners katika jedwali la ligi ya Uingereza

 . Mesut Ozil aliiweka Arsenal kifua mbele katika kipindi cha kwanza laki mshambulizi yasio koma ya Tottenham katika ngome ya Arsenal yalizaa matunda na kuiweka Tottenham kuibuka kidedea.

CHELSEA YAONGOZA LIGI KWA POINTI SABA


 Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kwamba haoni uongozi wa alama 7 juu ya jedwali la ligi ya Uingereza ni fursa ya timu hiyo kushinda ligi hiyo mwaka huu. The Blues iliishinda Aston Villa 2-1 siku ya jumamosi huku Manchester City Inayoshikilia nafasi ya pili katika jedwali hilo ikiangukia sare ya 1-1 dhidi ya Hull City.

 James Milner alifunga bao la Mancity lakini hakuisaidia timu yake kupunguza pengo lililopo kati yake na Chelsea katika uongozi wa Ligi. Manchester city Hull City ilikuwa ya kwanza kufunga bao kupitia mchezaji David Meyler. Everton na Liverpool nazo zilitoka sare ya 0-0 katika Merseyside Derby iliochezwa katika uwanja wa Goodison Park Haya hapa baadhi ya matokeo ya mechi zilizochezwa jumamosi

. Tottenham 2 - 1 Arsenal Aston Villa 1 - 2 Chelsea Leicester 0 - 1 Crystal Palace Man City 1 - 1 Hull QPR 0 - 1 Southampton Swansea 1 - 1 Sunderland Everton 0 - 0 Liverpool

MSIMAMO WA LIGI YA BARA BAADA YA MICHEZO YA JANA

RnTimuPWDLFAGdPts
1Azam FC126421710722
2YANGA12642137622
3POLISI MORO144731211119
4JKT RUVU145451414019
5RUVU SHOOTING145451010019
6MTIBWA SUGAR11461137618
7Coastal Union14464109118
8KAGERA SUGAR144641111018
9SIMBA SC133821311217
10MBEYA CITY1344599016
11NDANDA FC144371218-615
12MGAMBO SHOOTING12426611-514
13STAND UNITED14266917-812
14T. PRISONS131841012-211

LIGI KUU YA VPL KUENDELEA LEO

Mechi za leo 2015-02-08
16:00YANGA - : -MTIBWA SUGAR
MICHEZO INAYOKUJA
2015-02-11
16:00AZAM FCVs    MTIBWA SUGAR
16:00MGAMBO JKTVs    SIMBA SC