Jumapili, 8 Februari 2015

CHELSEA YAONGOZA LIGI KWA POINTI SABA


 Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kwamba haoni uongozi wa alama 7 juu ya jedwali la ligi ya Uingereza ni fursa ya timu hiyo kushinda ligi hiyo mwaka huu. The Blues iliishinda Aston Villa 2-1 siku ya jumamosi huku Manchester City Inayoshikilia nafasi ya pili katika jedwali hilo ikiangukia sare ya 1-1 dhidi ya Hull City.

 James Milner alifunga bao la Mancity lakini hakuisaidia timu yake kupunguza pengo lililopo kati yake na Chelsea katika uongozi wa Ligi. Manchester city Hull City ilikuwa ya kwanza kufunga bao kupitia mchezaji David Meyler. Everton na Liverpool nazo zilitoka sare ya 0-0 katika Merseyside Derby iliochezwa katika uwanja wa Goodison Park Haya hapa baadhi ya matokeo ya mechi zilizochezwa jumamosi

. Tottenham 2 - 1 Arsenal Aston Villa 1 - 2 Chelsea Leicester 0 - 1 Crystal Palace Man City 1 - 1 Hull QPR 0 - 1 Southampton Swansea 1 - 1 Sunderland Everton 0 - 0 Liverpool

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni