Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kuna kila sababu ya
mashabiki wa Simba kuendelea kumvumilia.
Amesema ana imani na kikosi chake kitakuwa na mabadiliko baada ya
muda, lakini uvumilivu ndiyo dawa.
“Tumekuwa na vipindi vya kupanda na kushuka, utaona mechi moja
tuko bora zaidi na nyingine tunashuka.
“Uvumilivu ndiyo jambo muhimu zaidi. Hatuwezi kufanikiwa kama leo
tutachanganyikiwa na kuanza kufanya vitu nje ya msitari.
“Sare na Coastal si tulichokitaka, lakini angalau hatujapoteza
mchezo tunaweza kuendelea kujipanga,” alisema Kopunovic raia wa Simba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni