Kocha
Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia wachezaji wake, dawa ya
kuondokana na kupoteza nafasi nyingi ni kuwa watulivu na kuachana na
presha ya mashabiki kwa muda.
Pluijm
raia wa Uholanzi, ameendelea kulizwa na wachezaji wake kupoteza nafasi
za kufunga na kusema wanaweza kuzitumia vema kama wakijiondoa katika
presha.
"Wachezaji
wanachanganyikiwa kwa kuwa presha ni kubwa sana, wako wanataka kufunga
kila mpira lakini wako ambao wanapata nafasi, lakini hawana utulivu.
"Yanga ni timu kubwa, presha ya mashabiki ipo juu na hii inawaathiri wachezaji.
"Nimezungumza
nao mara kadhaa, nimesisitiza suala la presha na kuwaambia mashabiki
wana haki yao katika kudai ushindi na mabao lakini wao wanapaswa kufanya
kazi yao kwa ufasaha kwa mujibu wa tulichojifunza," alisema.
Yanga
inashuka leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kucheza mechi yake ya
kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.